mara nyingine hivi ndivo huonekena mawinguni
SIRI YA UPINDE WA MVUA WINGUNI.
Upinde wa mvua ni ishara ya agano kati ya Mungu na nchi. Upinde unapoonekana winguni maana yake Mungu anakuwa amekumbuka agano lake kati yake na nchi aliloweka kwajili ya Nuhu. kwa namna hii tunaona upinde wa mvua umebeba kumbukumbu ya agano.
Mwanzo 9:13
“mimi nauweka upinde wangu winguni nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi.”
Kwaiyo tunapoona upinde wa mvua mawinguni moja kwa moja ni kumbukumbu ya agano aliloliweka Mungu na Nuhu ya kwamba hatoangamiza tena nchi kwa gharika na kila chenye mwili hakitoangamizwa tena kwa maji ya garika.
Tizama neno la Mungu (mwanzo 9:11)
“na agano langu nitalithibitisha nanyi, wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika wala hakutakuwa tena na gharika, baada ya hayo, kuiharibu nchi”.
Ukisoma mwanzo 9:1-17 utagundua kuwa baada ya Mungu kufanya agano na nuhu alizuia watu walioko katika nchi na vitu vyote vilivyo hai juu ya nchi kutopoteza uhai wake kwa njia ya maji ya gharika maana kabla ya hapo watu wake walikuwa wamefanya dhambi kupita kiasi basi akaamua kuangamiza kizazi chake cha kwanza nuhu akapata neema ya kuishi yeye na ndugu zake.
Kwanini Nuhu alipata neema ya kuishi?
Nuhu alipata neema hiyo kwasababu alikuwa tayari ni mwenye haki, nuhu alikuwa mtakatifu hakutenda dhambi ndiyo maana akahurumiwa na Mungu na kupitia yeye ndugu, wanyama na ndege wa angani na chochote chenye uhai kilihurumiwa na Mungu na kuokolewa toka mauti ya gharika iliyotokana na adhabu ya Mungu juu ya dhambi .
Chukua Biblia takatifu usome maana imesema haya wazi wazi katika kitabu cha (mwanzo 6:5-18) na utaelewa zaidi kila nilichosema apo.
Kwaiyo unapoomba kuhusu Mungu akuletee mvua hebu mwambie alete mvua kwa kiasi chake, mvua ambayo haitokufanya upoteze uhai,
Hata unapoona mvua ikinyesha kupita kawaida na pengine unaona mafuriko yakija au yakitokea nenda magotini tumia maandiko haya kumkumbusha Mungu juu ya agano lake aliloliweka juu ya nchi kati Nuhu na yeye maana alisema hakuna kitakachopoteza uhai kwasababu ya gharika.
Unapoomba sema na mbigu lakini pia usisahau kusema na aridhi maana aridhi ndiyo iliyokubeba wewe na vyote vyenye uhai, aridhi imebeba uhai wako aridhi imebeba agano kati yako na Mungu
Mwanzo 9:17
Mwambie Mungu akumbuke agano lake, unapoongea na mbingu uite upinde wa agano uonekane mawinguni ndipo Mungu atakumbuka kuwa alisema hakuna kitakachokufa kwa gharika ya maji..
hatutarajii kuona watu wakipoteza uhai kwa mafuriko kwaiyo mkumbushe Mungu atasikia (Isaya 43:26)pia (Isaya 59:1) ni wajibu wetu, maandiko yamesema wazi wazi Mungu akisema tumkumbushe.Mungu atakuponya wewe, atawaponya ndugu zako pia ataiponya nchi.
Asante sana mpendwa ambaye umeona vema kutembelea tovuti hii ya nehemiahollyservice kujifunza kuhusu nguvu au siri ya upinde winguni pale unapoonekana, endelea kufuatana nami na ili roho wa Mungu atakaponisaidia kujua mambo mengine kiroho basi tushitiki pamoja.
[…barikiwa sana ewe mtu wa Mungu…]
إرسال تعليق