KARIBU TUJIFUNZE NENO LA MUNGU KUHUSU 

NGUVU YA SHAUKU KATIKA IMANI

Shauku ni nini?

Ni kiu ya kufikia tumaini lako  au matarajio ya kuona jambo Fulani likitokea ama kutenedeka kwa namna ile na viwango vile au zaidi ya viwango  unavyofikri kutokana na imani ulionayo

Nguvu ya shauku ni msukumo unaokuwa ndani ya nafsi ya mtu mwenye shauku. Kama hakuna nguvu ya msukumo juu ya jambo unalotumaini jua shauku yako haijakamilika na kukamilika kwake ni kuwa na imani juu ya tumaini au matarajio ya jambo Fulani kutokea kwa mfano unashauku ya kuona uponyaji kama huna imani juu ya shauku hiyo huwezi kupambania matajio yako, na mojakwamoja kama huwezi kupambania kiu na tumaini lako basi jua ndani ya nafsi yako hakuna nguvu ya shauku na vilevile imani itazidi kuwa ndogo kila kukicha na mwisho tumaini litapotea.

Mwenye kiu hutafta namna ya kuikata kiu ambayo tunaoina katika shauku, mwenye shauku hazuiliwi na chochote kufanya jambo ama kupokea jambo  atapambana mpaka aifiki hatima ya shauku yake  kwa lugha nyepesi akate kiu yake.

Ø  Zaburi 107:5-7

“ 5 waliona njaa wakaona kiu nafsi yao ilikuwa ikizimia ndani yao. 6 wakamlilia BWANA katika dhiki zao, akawaponya. 7 akawaongoza kwa njia ya kunyoka, wapate kwenda mpaka mji wa kukaa”

hawa watu  walikuwa wana njaa walikuwa na kiu katika nafsi zao ndipo wakamlilia BWANA katika taabu yao na kwasababu ndani ya nafsi zao walikuwa na kiu ya kupata shibe walikuwa wanahitaji kupata makazi ya kudumu kwasababu wamechoka kutanga-tanga ndipo wakamlilia Mungu nae akawasikia akawaponya akawainua katika njia iliyonyooka mpaka mji wa kukaa.

Haleluyaa… haleliyaa…

Kinachowafanya walie sio njaa bali ni nguvu ya shauku ndani ya nafsi zao ya kupata chakula,.. ya kupata makazi.. ili kuondokana na dhiki zao ndipo wakasikika

Kuna watu wanapokuwa katika dhiki zao wanaishia kulaumu, wanalaumu hata viongozi wao na kumuasi Mungu badala ya kumtafta ili awaponye

Angalia neno  la Mungu linaonyesha wazi wazi  juu ya habari ya wana wa Israeli wanavvyolaumu viongozi wao musa na haruni kwa sababu ya taabu wanazokumbana nazo toka walipotoka katika nchi ya misri

Ø  Kutoka 16:2 “na mkutano mzima wa wana wa Israeli ukawanung’unikia Musa na Haruni, huko barani”. Ukiendelea kusoma msitari wa tatu utaona wanadai angalau wangalikufa wakiwa bado misri kuliko kuja huku kufa kwa njaa.

Ni hatari sana Kama umeokoka na huna shauku ya kumtafta Mungu na badala yake unaonyesha hali ya kukata tamaa. Kama hauna  shauku ya namna hiyo na umeokoka fahamu kuwa wokovu wako si wa faida maana hautajua siri za Mungu na utaipoteza haki yako itokayo kwa BWANA maana neno la mungu katika

Ø  ( warumi 5:1 linasema “basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu kristo,”.)

Tunaona katika somo hili ndani ya imani  ndiko kuna chemichemi ya haki na amani  katika njia ya bwana wetu yesu kristo. Kuna kupata haki katika imani kwasababu imani imebeba shauku na shauku katika imani hai huwa ina nguvu ya kuyaona  yale unayoyatarajia katika imani maana neno imani ni bayana ya mambo yote yatarajiwayo kuonekana.

Kwa lugha nyepesi bila nguvu ya shauku ndani yako huwezi kuipata haki yako.

Hivyo....

Mungu huguswa na shauku  walionayo watu wake kumuelekea yeye kwa lengo la kupata msaada kwaiyo tumia iyo nguvu kumuita BWANA ili akusaidie maana usipomuita hatokuja kuleta msaada hata kama anazijua shida zako.

Ø  Mungu  anasubiri wewe mwenyewe useme hitaji lako sawa sawa na ilivyoandikwa katika biblia takatifu

Ø  (Isaya 45:11 “BWANA, mtakatifu wa Israeli, na muumba wake asema hivi niulize habari za mambo yatakayokuja, mambo ya wana wangu, na habari ya kazi ya mikono yangu; haya niagizeni.”)

 Mungu ametoa wito wa wewe kumuuliza juu ya kazi ya mikono ya halafu ukisha muuliza muagize. Unaweza ukawa una kiu ya kuona uponya lakini hauufikiii, una shauku  ya kuona neema yake ikikutokea lakini unaona kama imechelewa hebu muulize maana hilo ni swala la kazi ya mikono yake  halafu umuagize amekupa hiyo nafasi pia ila agiza sawa na nguvu ya shauku katika imani

Mahali pengine biblia takatifu neno la Mungu inakupa nafasi ya kuhojiana nae kisha ueleze hitaji lako usisubiri muujiza ujilete tu tumia nguvu ya shauku katika imani juu ya jambo unalohitaji maana haki yako ndiko itakapotokea,

Ø  Angalia neno la Mungu katika kitabu cha Isaya 43:26 “unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo  yako, upate kupewa haki yako.” Neno la mungu limeonyesha wazi wazi juu ya kusema na mungu ili upate haki yako na limetupa  muongozo katika mambo matatu na unaweza ukachagua katika kuomba au ukayatumia yote,.. mambo hayo ni:-

Ø  Kumkumbusha Mungu

Ø  Kuhojiana nae

Ø  Kueleza mambo yako

Lengo la kufanya hayo yote ni kuipata haki yako ilioko katika imani yako kwaiyo jifunze kutumia maandiko ukiambatana na nguvu ya shauku katika imani yako na Mungu atakuinua atakukumbuka kama tulivoona katika zaburi ya 107 mtari ule wa 6

Kuna watu huwa hawana pa kuishi ila hawamwambii bwana, kuna watu wana migogoro ya kifamilia, kiukoo, kikabila, hata kitaifa kwa mfano magonjwa yanayoweza kulikumba taifa na mwisho wa siku linakuwa tatizo kubwa tena linaloathiri hata uchumi wa nchi ila hawasemi,.. wamekaa kimya, wanatamani kuwa huru kutoka katika kesi mbali mbali za kidunia lakini hamuiti Mungu hiyo ni hatari sana na unaweza usione mungu akitokea kwasababu tu haujamkumbusha na kumlilia yeye aliye juu ambayo katika yeye kila kitu kipo chini ya uweza wako.

Sasa tumia shauku ilioko ndani ya nafsi yako ya kupata kile ulichokikosa ili ukipate na hatimae utukukufu wa BWANA  utadhihirika

Kama hauna shauku ndani yako hilo nalo ni tatizo hebu fanya toba na uamini juu ya toba kwanza ndipo utaipokea nguvu ya shauku katika imani baada ya hapo utaweza kuomba na mungu atakusikia maana neno lake lipo wazi katika biblia tungalie kitabu cha isaya

Ø  Isaya 59:1

Ø  “tazama mkono wa BWANA haukupunguka hata usiweze kuokoa wala sikio lake sio zito hata lisiweze kusikia”

hawezi kukusikia kama huna nguvu ya shauku na una dhambi kwaiyo tumia damu ya yesu katika kufanya toba ndipo uombe jambo lolote atakusikia nawe utauona mkono wa bwana ukikutetea na kukuongoza katika njia nyofu kama tulivoona katika zaburi 107:7

ubarikiwe na bwana

kwa mawasiliaano zaidi tunaweza kuwasiliana kupitia namba ya simu

Ø  0742786378

Ø  0628305265

Ama kwa barua pepe

Ø  Wismangeorge8@gmail.com

Asante kwa kutembelea tovuti yetu ya nehemiahollyservice ambayo ni wgservice.blogspot.com

Karibu tena tuendele kujifunza neno la Mungu pamoja pia nakusihi usisahau kutoa maoni yako na tutayafaniya kazi kupitia tovuti yetu ya nehemiahollyservice na Mungu atakubariki sana kwa kufanya hivo.

Post a Comment

أحدث أقدم